Sunday , 30th May , 2021

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kupitia kwa Naibu Waziri wake Dkt. Godwin Mollel ametembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuagiza kumalizwa kwa changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa.

Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel

Akiongea kwenye mahojiano maalum na East Africa Television, Dkt. Mollel amewataka wafanyakazi wa viwanja vya ndege kuzingatia uzalendo maana wao ndio wamebeba taswira ya nchi.

''Nimeenda KIA nimeambatana na Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkoa na nimewaagiza tufuate taratibu za Shirika la Afya Duniani WHO ambazo tumekubaliana lakini pia taratibu zetu zikiwemo za usalama na pia viwepo vyumba zaidi ya 10 vitakavyosaidia kuhudumia watu,” ameeleza Dkt. Mollel.

Zaidi tazama Video hapo chini