
Pep Gurdila kushoto na Thomas Tuchel kulia
Mchezo huu unazikutananisha timu mbili kutoka England Manchester City na Chelsea utachezwa katika dimba la Dragao huko Porto, Ureno. Mtanange huu utaanza majira ya Saa 4:00 Usiku kwa Saa za hapa nyumbani.
Usikuwa wa leo itakuwa ni mara ya nane kocha Pep Guardiola na Thomas Tuchel wanakutana kwenye michezo rasmi ya masindano, michezo saba ya mwisho kukutana Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameshinda mara nne dhidi ya Tuchel ambaye yeye ameshinda mara mbili tu huku wakiwa wametoka sare kwenye mchezo mmoja.
Mara ya kwanza makocha hawa kuchuana kimbinu ilikuwa mwaka 2013 kwenye ligi kuu ya nchini Ujerumani Bundesliga ambapo Pep alikuwa kocha wa Bayern Munich na Tuchel alikuwa akikinoa kikosi cha Mainz 05, lakini baadae Tuchel alihamia Dortmund ya ujerumani pia. wakiwa katika ardhi ya ujerumani walikutana mara tano na Pep alishinda mara nne wakati Tuchel akiambulia sare moja.
Michezo pekee aliyomfunga Pep Guardiola kocha Thomas Tuchel ameshinda akiwa na kikosi cha Chelsea na michezo yote hiyo ni ndani ya msimu huu wa 2020-21, mchezo mmoja wa Ligi Kuu ambao Chelsea ilishinda kwa mabao 2-1, na mchezo mwingine ulikuwa wa hatua ya nusu fainali ya kombe la FA mchezo ambao The Blues ilishinda kwa bao 1-0.
Lakini pia kocha Pep Guardiola katika maisha yako ya ukocha amepoteza michezo mingi zaidi dhidi ya Chelsea amefungwa mara saba, pia amepoteza michezo miwili mfululizo iliyopita dhidi ya matajiri hao wa jiji la London.
Pep Gurdiola ameshatwaa ubingwa wa michuano hii ya Ligi ya mabingwa barani ulaya mara mbili mwaka 2009 na 2011 akiwa na kikosi cha FC Barcelona lakini ni kwa mara ya kwanza ataiongoza timu kwenye mchezo wa fainali leo usiku baada ya taklibani miaka 10 tangu mara ya mwisho kufika katika hatua hii. Thomas Tuchel hajawahi kutwaa ubingwa wa michuano hii, lakini ni msimu wa pili mfululizo anatinga hatua ya fainali msimu uliopita alifika hatua hii akiwa na kikosi cha PSG ya Ufaransa lakini alipoteza mchezo kwa kufungwa bao 1-0 na Bayern Munich.