Saturday , 29th May , 2021

Katika kupambana na uhalifu nchini Serikali imetangaza miezi mitatu ya operesheni kali lengo ikiwa kupambana na uhalifu huku zaidi ya watuhumiwa sitini wakishikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene alipotembelea Kituo cha Polisi cha Kati kuzungumza na watuhumiwa hao waliokamatwa na Jeshi la Polisi, nakumpongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa huo RPC Gilles Muloto kwakazi walioifanya yakuwakamata wahalifu.

“Msako wa aina hii sio nyinyi tu mikoa yote msako unaendelea na hakuna kusimama msako mpaka miezi mitatu, nashukuru RPC kwa kazi nzuri hii siku mbii tu, tutatafauta magereza pa kuwaweka watatosha hii habari yakusema msongamano halafu watu tunawaachia wanaenda mtaani wanaendelea kutuumiza tusifanye shughuli zetu haiwezekani,” amesema Mhe. Simbachawene.

Akizungumzia juu ya wafungwa waliotoka kwa msamaha na kurudi akufanya uhalifu amesema uhalifu hauna nafasi katika nchii hivyo hawawezi kuhalalisha uhalifu kwani sheria lazima ifuate mkondo wake.

“Matukio ya kukaba, kubaka, kuvunja nyumba, kuiba na kunyang’anya kwenye bodaboda yamekuwa mengi sana na ni kundi hili hili ndio mmeamua hamtaki kufanya kazi halali mnataka kujihusisha na masuala ya uhalifu nchi hii uhalifu hauna nafasi,” amesema Mhe. Simbachawene.