
Kombe la CAF Super Cup 2020
Wawili hao wanaokutana kwa mara ya kwanza, wanakutana kikanuni baada ya Al Ahly kuwa mabingwa wa michuano ya klabu Bingwa Afrika na RSB Berkane akiwa bingwa wa kombe la Shirikisho Afrika wote kwa msimu wa mwaka 2019 hadi 2020.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika kabla ya msimu huu kuanza lakini kutokana na Covid-19 ikalazimika kusogezwa mbele na hatimaye kitapigwa leo.
Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane amesema anawapa nafasi kubwa Berkane kufanya vizuri kutokana na wao kuwa na uchovu mkubwa baada ya kucheza michezo minne mikubwa na kusafiri mbali mrefu bila kupumzika vya kutosha.
“Tumecheza michezo minne mikubwa na tunakuja kucheza mchezo watano na kusafirisha mfululizo, tena kutoka Cairo hadi Johannesburg na pia hadi Doha, itakuwa ngumu sana kwetu.”
“Lakini tutajaribu kuhakikisha tupo tayari kwa ajili ya mchezo kiakili na kimwili kwani hatupo kwenye nafasi nzuri kama Berkane ambao wamesafiri kutoka Casablanca ambapo si mbali na walipo”
Kwa upande wa kocha wa Berkane, Juan Pedro Benali amesema, “Tunawaheshimu sana Al Ahly, lakini hakuna anafsi yeyote ya kuwaogopa. Huu ni mchezo wa mpira wa miguu na tuna nafasi yetu pia. Tunapaswa kuwa tayari kwa mazingira yeyote na tutakuwa tayari”.
Shirikisho la soka Afrika CAF na lile la chini Qatar yamekubaliana kuruhusu asilimia thelathini ya uwezo wa uwanja huo wa kuchukua watu 12946 ambayo ni 3884 kuingia uwanjani na kutazama mchezo huo huku wakiendelea kuchukua tahadhari ya Covid-19.
Kihistoria Al Ahly wametwaa kombe hilo mara sita wakitafuta kutwaa kwa mara ya saba wakati ambao Berkane atakuwa ana haha kusaka taji lake hilo kwa mara ya kwanza.