
Picha ya Tundaman na MO Dewji upande wa kulia
Licha ya kuwa wanachama wa timu moja ya Simba, Tundaman amesema yeye na Bilionea MO Dewji ni watu wa karibu sana na anaweza akampigia hata simu kupiga stori.
"Boss MO Dewji anajua mimi ni shabiki wa Simba damudamu, ni mshikaji wangu kuna muda mwingine anaweza kunipigia simu anauliza uko wapi njoo tupige story, upendo anaonionyesha mpaka kuna muda mwingine naogopa, anasemaga wewe sio rafiki yangu wewe ni ndugu yangu hii kauli huwa inanitesa sana".
"Kuna watu wanakuwa sehemu kwa ajili ya kupiga hela ila kuna watu wako sehemu kwa ajili ya mapenzi, mimi siishabikii Simba ili nifaidike, nipo pale kwa sababu nina mapenzi nayo" ameeleza Tundaman
Kwa sasa msanii huyo anatamba na wimbo wake mpya wa 'True love' ambao amemshirikisha MO Dewji.