Wednesday , 26th May , 2021

Mpemba mmoja Nedy Music amesema hana ugomvi na Ommy Dimpoz ila kitendo cha Ommy  kuonesha au kutoonesha sapoti kwake baada ya kutoka kwenye lebo yake PKP ni matakwa yake binafsi.

Picha ya msanii Nedy Music kushoto, kulia ni Ommy Dimpoz

Nedy Music amesema anamuheshimu Ommy Dimpoz kwa sababu ni msanii ambaye amempigania kwenye mishe za muziki na amemfungulia njia ya kufika alipo kwa sasa na kwenye lebo yake mpya ya Fine Boy Music.

"Sasa hivi Nedy yupo na lebo ya Fine Boy Music ambayo anafanya nayo kazi, Ommy Dimpoz atabaki kuwa mtu mwenye thamani kubwa kwangu, amenipigania na kunifungulia njia kwenye muziki wangu mpaka kufika hapa

"Nilikuwa chini ya Ommy Dimpoz sasa hivi sipo huko, kuonesha au kutokuonesha sapoti ni matakwa yake binafsi hatuliweki kama ni ugomvi kwa sababu bado upendo upo, namzungumzia vizuri na naamini anajivunia kwa ninachokifanya" ameeleza Nedy Music 

Nedy Music chini ya PKP ya Ommy Dimpoz alitoa nyimbo mbili ambazo ni rudi ft Christian Bella na usiende mbali ft Ommy Dimpoz.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video