
Msanii Marioo
Wimbo huo uliendelea kumuweka katika nafasi nzuri kimuziki kutokana na mapokezi yake kuendelea kuwa makubwa, huku video yake ilifanyika mjini Morogoro na Dar es Salaam na kuongozwa na Frank Papushka na Hanscana brand, huku na audio ilitayarishwa na Kimambo.
Kwasasa Marioo ni miongoni mwa wasanii wa Bongo wenye nguvu kubwa ya ushawishi ambapo amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wakubwa wa nje ya Tanzania kama Sho Madjozi, Bontle Smith, Skales.