Sunday , 30th Nov , 2014

Mvua zilizoambatana na upepo zimeezua paa la kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi cha Tosamaganga kilichopo nje kidogo ya manispaa ya Iringa na kusababisha hasara ya karibu shilingi milioni 150.

Moja ya jengo la Kituo kilichoezuliwa kutokana na mvua

Mvua zilizoambatana na upepo zimeezua paa la kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi cha Tosamaganga kilichopo nje kidogo ya manispaa ya Iringa na kusababisha hasara ya karibu shilingi milioni 150.

Baadhi ya wahudumu na walezi wa watoto katika kituo hicho akiwemo mwalimu wa shule ya chekechea ya kituo cha Tosamaganga Sista Secilia Said Filimbi wamesema upepo huo umesababisha hasara kubwa na kulazimu kituo kufunga shule ya chekechea kutokana na madarasa mawili ya shule hiyo kuezuliwa.

Kwa upande wake mmoja wa masista wanaofanya kazi katika kituo hicho Sista Maria Mbilinyi ameiomba serikali, taasisi na watu binafsi kujitolea kusaidia kituo hicho ili kukirudisha katika hali yake ikiwa ni pamoja na kuwarudisha mapema watoto shuleni ambao wamelazimika kufunga shule kwa muda kutokana na madarasa yao kuezuliwa.