Monday , 24th May , 2021

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luiz Enrique hajamjumuisha nahodha wa kikosi hicho Sergio Ramos kwenye kikosi cha wachezaji 24 alichokitaja leo kuelekea fainali mataifa barani ulaya Euro 2020.

Sergio Ramos

Luiz Enrique amesema aliongea na Ramos jana Jumapili kwa njia ya simu kumjuza kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoenda kwenye fainali za Euro,

"Ningependa kutuma ujumbe kwa Sergio Ramos, nahodha wetu, ambaye hayumo kwenye orodha kwani hakuweza kushindana tangu Januari, hakuwa katika hali nzuri, hakuweza kufanya hata mazoezi. Ni uamuzi mgumu lakini ni jambo zuri kwa timu." Amesema Enrique

Ramos mwenye umri wa miaka 35 ndio mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi kwenye timu hiyo amecheza michezo 180 lakini pia ni mfungaji namba nane (8) kwenye orodha ya wafunaji wa muda wote wa Hispania.

Lakini pia katika kikosi hicho kocha Luiz Enrique amemjumuhisha beki wa kati wa Manchester City Aymeric Laporte ambaye amebadilisha uraia wake kutoka Ufaransa na sasa Hispania.

Kikosi kamili cha Hispania kilichotangazwa leo.

Magolikipa: Unai Simon (Athletic Bilbao), David de Gea (Manchester United), Robert Sanchez (Brighton)

Mabeki: Pau Torres (Villarreal), Aymeric Laporte (Manchester City), Diego Llorente (Leeds United), Eric Garcia (Manchester City), Jordi Alba (Barcelona), Jose Gaya (Valencia) Cesar Azpilicueta (Chelsea)

Viungo: Sergio Busquets (Barcelona) Rodri (Manchester City), Thiago Alcantara (Liverpool), Pedri (Barcelona), Marcos Llorente (Atletico Madrid), Koke (Atletico Madrid), Fabian Ruiz (Napoli)

Washambuliaji: Gerard Moreno (Villarreal), Ferran Torres (Manchester City), Mikel Oyarzabal (Real Sociedad), Alvaro Morata (Juventus), Dani Olmo (RB Leipzig), Pablo Sarabia (Paris Saint-Germain), Adama Traore (Wolves)