Saturday , 29th Nov , 2014

Staa wa filamu Bongo, Emmanuel Myamba maarufu zaidi kama Pastor Myamba amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao atajikita katika kutengeneza filamu zinazohusiana na maswala haya ya ndoa kutokana na kugundua kuwa ni taasisi inayopigwa na changamoto sana.

Pastor Myamba

Myamba ambaye binafsi ameanza maisha ya ndoa hivi karibuni amesema kuwa, atasuka filamu hizi katika mtindo ambao utawagusa kila mmoja katika ndoa, kurejesha vicheko, kuibua kilio lengo likiwa ni kusaidia kuyasongesha mahusiano haya kuvuka changamoto zake za kila siku.

Tags: