Thursday , 20th May , 2021

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeeleza kuwa huduma ya manunuzi ya LUKU sasa inapatikana kupitia mitandao ya Simu na Benki.

Mita inayotumia umeme wa LUKU

Aidha imeongeza kuwa ofisi zote za TANESCO Wilaya na Mikoa zitaendelea kutoa hudumu kwa saa 24.

Imesisitizwa kuwa wataalamu wake wanaendelea kuangalia ufanisi wa mifumo ya manunuzi.

Kwa upande mwingine Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Mei 20, 2021 amezungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi  na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwenye Makao Makuu ya zamani ya Shirika hilo Ubungo jijini Dar es salaam.