Monday , 17th May , 2021

Kwa mara ya kwanza msanii Whozu amejibu taarifa zinazosemekana mitandaoni kwamba mpenzi wake Cappiccuno Tunda ni mjamzito kwa kusema mpenzi wake huyo sio mjamzito na hakuna kitu kama hicho.

Whozu na mpenzi wake Tunda

Pia Whozu amesema tayari ameshaandaa jina endapo akipata mtoto ambapo atamuita Lora kwa sababu analipenda sana na tayari ameshachora tattoo ya jina hilo kwenye mwili wake.

"Lora ni jina ambalo nalipenda sana tangu nikiwa nasoma natamani kwenye maisha yangu nikipata mtoto wa kwanza au wa pili lazima aitwe Lora, Tunda hana ujauzito ila hapa nimeongea tu" amesema Whozu 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.