ACT-Wazalendo imebainisha hayo kupitia taarifa iliyotolewa leo na Naibu Katibu Habari, Mawasiliano ya Umma na Uenezi, Janeth Rithe ilieleza kuwa helikopta waliyoikodisha si salama na bado haijafanyiwa matengenezo na hivyo kutokuwa salama kwa matumizi.
Taarifa ya ACT-Wazalendo imeeleza kuwa mikutano yote sita iliyokuwa ifanyike leo katika majimbo hayo, itafanyikia kama awali ilivyopangwa ila kwa kutumia msafara wa magari.