
Msanii Isha Mashauzi
Isha Mashauzi amesema alikutana na mume wake huyo huko Zanzibar baada ya kufukuzwa nyumbani kwao na mama yake mzazi
"Nilifukuzwa nyumbani na mama baada ya kukutwa na rafiki yangu aliyekuwa amelewa,nikaenda kuishi Zanzibar, huko nilimpata baba mtoto wangu na baada ya hapo ndiyo ikabidi nirudi nyumbani tena kwa ajili ya ndoa, ngawa ndoa haikua riziki"
"Nilivyoolewa ndoa ya pili, nilikuwa nampenda sana mtoto wa mume wangu na mpaka sasa hivi ameolewa, nilimlea kwa misingi niliyofundishwa mimi" ameeleza Isha Mashauzi