Thursday , 6th May , 2021

Mchezaji wa zamani wa  Yanga na Simba Haruna Moshi amesema kuwa  maandalizi ya mechi ya Dar es salaam Derby   yanakuwa ya kipekee kutokana na utofauti wa  ukubwa wa mtanange huo ambao unazikutanisha timu zenye mashabiki wengi nchini ambao ni watani wa jadi. 

Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Haruna Moshi 'Boban'.

 

Akizungumza na EATV Boban amesema yoyote atayekuwa amejianda vizuri atashinda ila ni ngumu kutabiri yupi atashiinda kutokana na ugumu wa mechi hizo.

''Mandalizi ya Simba na Yanga yanakuwa ya kipekeake kutokana na mara nyingi viongozi wanakuja kambini  kukaa na sisi kutupa maneno namna gani ambayo tutacheza na pia kutupa ahadi iwapo tutashinda". 

Hata hivyo  Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa stars' Boban ijumaa ya wiki hii atahitimu mafunzo ya kozi ya FIFA ya Grassroots ambayo  yanasimamiwa  na mkufunzi kutoka katika shirikisho la mpira wa miguu nchini Raymond Gweba .