
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Geita Henry Mwaibambe
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Geita Henry Mwaibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanaume huyo aliamua kufanya vitendo hivyo mara baada ya yeye kwenda kliniki na mke wake na ndipo alipogundulika kama ni mwathirika wa ugonjwa huo.
"Mtoto amepata jeraha kubwa tumboni na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Geita, huyu mwanaume alikuwa anakaa kwa mwanamke na mwanamke alimuomba ruhusa kwenda nyumbani kusalimia sasa tunadhani huyu mwanaume alihisi anaenda kuwaambia wazazi wake ili aachwe kwa sababu mwanaume alikuwa hana kazi ya maana", amesema Kamanda Mwaibambe.
Aidha kamanda Mwaibambe amewaasa wananchi kutoa taarifa juu ya vitendo vya kikatili vinavyotokea ndani ya familia ili kuvikomesha.