Wednesday , 19th Nov , 2014

Michuano ya Mpira wa Kikapu ya Raia wa China waishio Tanzania imeanza leo katika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo inatarajiwa kumalizika Novemba 29 mwaka huu.

Makamu wa Rais wa BD,Richard Julls

Akizungumza na East Africa Radio, Mkamu wa Rais wa Chama Cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es salaam BD, Richard Julls amesema michuano hiyo inayoshirikisha timu 10 kutoka makampuni mbalimbali inalengo la kukutanisha raia hao waliopo hapa nchini.

Julls amesema michuano hiyo ambayo imeingia mwaka wa tatu tangu kuanzishwa haina ushindani mkubwa sana kutokana na wachezaji wengi kutokuwa na mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo lakini wanaamini mashindano hayo yatazidi kutambulika kadri timu hizo zitakavyozidi kuonesha ushindani katika mashindano mengine yanayofuata.