
Mwalimu wa mahusiano na ndoa, Rosemary Mallya
Rosemary ameyasema hayo hivi karibuni kwenye kipindi cha DADAZ cha East Africa Television, kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kuongeza kuwa mwanamke aliyemfumania naye walikuwa wanafahamiana na wanatoka 'out' kwani alikuwa akimchukulia kama rafiki wa kawaida.
"Mimi nilikuwa kwenye ndoa ambayo ni ngumu sana nimeteseka sana, nilikuwa kwenye ndoa ambayo unajua kabisa mume wako ana mwanamke kabla hamjaingia kwenye ndoa halafu mpo kwenye vikao vya mwisho vya harusi, unafanyaje, unatokaje sasa unawadhalilisha wazazi wako unaanzaje kuwaambia wazazi wako kama siitaki tena hii ndoa nikasema potelea pote nitaolewa,"amesema Rosemary
"Nimeolewa Oktoba na Desemba nikamfumania mume wangu, nikaja kugundua kwamba mwanamke ambaye mimi natokaga naye kila siku na mume wangu na marafiki zangu kumbe ni mke mwenzangu na huyo mwanamke alikuwa ni rafiki wa mume wangu, katika kutatua magumu ya ndoa yangu nilifanya kila kitu," ameongeza kusema.
Tazama video hapa