Friday , 14th Nov , 2014

Shetta, rapa anayefanya vizuri katika muziki Bongofleva, amesema kuwa kufunga kwake mwaka huu wa 2014 kutakuwa na uzito wa aina yake hasa akizingatia mafanikio makubwa ambayo ngoma yake ya Kerewa pamoja na video imempatia.

wasanii wa bongofleva nchini Shetta akiwa na Diamond

Shetta ameiambia eNewz kuwa kazi hii imeweza kuvifikia vituo vikubwa vya kimataifa na hivyo kumtoa ngazi moja hadi nyingine kisanaa, na vilevile msanii huyu amesema Shikorobo ndiyo kazi yake mpya ambayo itamhusu yeye na pengine msanii mkubwa wa kimataifa ambaye hakuwa tayari kumtaja.