Anthony Joshua
Tyson Fury amesema, ''nataka kupigana na Joshua, nimpige ndani ya raundi tatu na nadhani nitamwonesha ubora mkubwa uliopo ndani yangu''.
Hata hivyo bondia wa Uingereza Anthony Joshua mwenye miaka 31, amemjibu Fury kwa kusema, ''imekuwa vizuri kama anataka kupigana, ni habari njema angalau sasa naweza kuwa na uhakika wa kukutana naye uliongoni''.

Tyson Fury
Pambano hilo ambalo linatajwa kuwa huenda likafanyika mwezi Machi mwaka 2020, litakuwa ni pambano la kwanza kuwakutanisha mabondia wanaomiliki mikanda yote ya uzito wa juu ambayo ni IBF, WBA na WBO kwa Joshua na WBC kwa Tyson Fury.
Usiku wa kuamkia leo Desemba 13, 2020, kwenye uwanja wa Wembley nchini Uingereza, Anthony Joshua alimpiga kwa KO raundi ya 9 Mbulgaria Kubrat Pulev.







