Msanii Stamina wakati anatambulishwa kwenye lebo yake mpya ya Akida OG
Boss Akida OG amesema ameamua kuchukua msanii huyo kwa sababu mke wake mkubwa anamfuatilia, kumpenda na kumtajataja sana na yeye kwakuwa anampenda mke wake akaamua kumsaini ili afanye naye kazi.
Tayari lebo hiyo ina jumla ya wasanii wanne kwa sasa ambao ni Rhino King, Mkali Wenu, Official Nai na Stamina Shorwebwenzi.
Kwa upande mwingine msanii wa BongoFleva Ommy Dimpoz amepata shavu la kusainiwa kwenye lebo kubwa Africa ambayo inajulikana kwa jina la 'Sony Music Africa' ambayo ipo nchini Africa ya Kusini.