Friday , 7th Nov , 2014

Msisimko mkubwa umeendelea kupanda kutokana na Tamasha la Karibu Music litakalofanyika huko Bagamoyo kuanzia siku ya leo ambapo hii itakuwa ni nafasi nyingine ya kuutangaza zaidi muziki wa Live na wenye vionjo vya Kiafrika katika ngazi ya kimataifa.

tamasha la muziki la Karibu Music nchini Tanzania

Wasanii mbalimbali wakiwemo Prof, Jay, Barnaba Boy, Juma Nature na wengineo wengi wamepanga kuimba nyimbo zao mbalimbali na pia kuonesha aina ya muziki wa Live na wa asili kwa kutoa burudani kuanzia kwa watoto mpaka watu wazima.

Tamasha hili linafanyika kwa siku Tatu mfululizo kuanzia leo mpaka Jumapili likiambatanisha Burudani ya muziki na semina juu ya sanaa hii kwa washiriki.