Tuesday , 13th Oct , 2020

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Wallace Karia ameunda kamati ya ushindi ya timu ya Taifa (Taifa Stars).

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara(Kushoto) na aliyekua Mkuu wa Idara kama hiyo katika Klabu ya Yanga, Jerry Muro enzi wakitaniana .

Kamati hiyo itaongozwa na Ghalib Said Mohamed wakati Makamu wake ni Salim Abdallah huku Katibu wa Kamati hiyo ni Hersi Said.

Wajumbe walioteuliwa ni Abdallah Bin Kleb, Anitha Rwehumbiza, Beatrice Singano, Christine Manyenye, Farid Nahdi na Feisal Abri.

Wengine ni Farough Baghozah, Haji Manara, Jerry Muro, Mohamed Nassor, Nandi Mwinyombella, Patrick Kahemele na Philemon Ntahijala.

Ikumbukwe Taifa Stars inajiwinda na michezo miwili ijayo dhidi ya Tunisia ambayo ni ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika itakayoanza kuchezwa Novemba 13 mwaka huu kabla ya kurudiana wiki moja baadaye.