Monday , 12th Oct , 2020

Mgombea urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kuboresha mfumo wa utumishi wa serikali ikiwemo kuongeza mishahara na kulipa posho stahiki kwa wafanyakazi.

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza hii leo Oktoba 12,2020 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Ditia Pemba, amesema kuwa ataongeza mshahara kutoka shilingi za Kitanzania laki tatu hadi laki tano.

''Nitaboresha utumishi na mfumo wa utumishi wa serikali pamoja na vikosi vya SMZ na tutarejesha posho zote ambazo wafanyakazi wanastahili kupewa'', amesema Maalim Seif

''Mwaka wa kwanza nitakapoingia madarakani nitaongeza mshahara kutoka laki tatu hadi laki tano na hadi namaliza miaka yangu mitano kima cha chini hakitapungua laki saba na mia tano'', ameongeza.

Aidha mgombea huyo amewataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi ili kupata kiongozi ambaye atasimamia haki na kuleta maendeleo