
Kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Jonas Mkude katika moja ya mechi ya Taifa Stars.
Julio amesema kwa bahati mbaya sana Mkude aliondolewa kwa kadi ya pili ya njano dakika ya 85 wakati timu ikiwa bado inamuhitaji na ndipo Burundi walitumia mwanya huo kuongeza jitihada zilizowasaidia kuandika bao hilo.
''Unajua hakuna kitu kizuri kama nidhamu kwenye mpira, kwa kweli tumefungwa kwa sababu ya pengo la Jona Mkude, sisi wachezaji wetu hawajui jinsi ya kuziba pengo la mchezaji fulani anavyotolewa na hawajui nini wafanye.
Tulikua kwenye shinikizo kubwa baada ya hapo, na Burundi walikua wanataka washinde na wapande kwenye viwango vya FIFA.
Siku nyingine mchezaji yoyote wa timu ya taifa akicheza, anapaswa kujua amebeba bango la nchi, kwa hiyo unapoingia uwanjani lazima ajue majukumu yake na lazima wacheze kwa kujitolewa, lakini wakicheza kama wapo kwenye bonanza hatuwezi kufanikiwa''
Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Tunisia utakaopigwa Novemba 13 ugenini kabla ya kurudiana wiki moja baadae.