
Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Euegene Kabendera
Akizungumza hii leo na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, mgombea huyo amesema kuwa anafahamu kuwa jimbo hilo linakabiliwa na changamoto ya ajira na kudai kuwa vijana wengi wengi wa Ubungo hawana ajira na kuahidi kurudisha viwanda vilivyokufa ili kuondoa tatizo hilo.
''Jimbo la ubungo lilikuwa na viwanda vingi kama urafiki lakini sasa hivi vimedorora na vingine vimefungwa tunahitaji mtu atakayepiga kelele kwa sababu vile viwanda bado maeneo yapo tunaweza kuleta wawekezaji vile viwanda vikafufuliwa'' amesema Kabendera
Aidha amesema njia hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya ajira ambapo pia ameahidi kutoa mikopo ambayo itawasaidia kujikomboa kiuchumi