Thursday , 8th Oct , 2020

Nyota wa Tanzania, Kelvin John ''Mbappe'' ameorodheshwa kwenye jarida maarufu Duniani la michezo The Guardian la Uingereza kama moja ya chipukizi hatari hapo baadae.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Kelvin John akiwa mazoezini.

Mshambuliaji huyo kwa sasa yupo katika chuo cha ''Brook House College Football Academy ''kilichopo Uingereza, amekua akionyesha kiwango bora tangu aanze kuonyesha uwezo wake katika michuano ya Copa Cocacola kwa muda mrefu tangu akiwa kinda .

Wachezaji wengine waliotajwa kuwa watakua tishio zaidi Duniani kwenye Jarida hilo ni pamoja na Israel Salazar (Real Madrid), Nico Serrano ( Athletic Bilbao), Mateja Bacanin ( Red Star Belgrade).

 

Wengine ni Luka Cveticanin (FC Vozdovac), Benjamin Sesko (RB Salzburg), Bryno Iglesias (Real Madrid), na Emil Roback ( Ac Milan).