Thursday , 8th Oct , 2020

Nyota Namba moja duniani katika mchezo wa tenisi Novak Djokovic, alitinga nusu fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa, baada ya kumshinda Pablo Carreno Busta.

Novak Djokovic (Pichani) akipatiwa matibabu wakati wa mchezo wake wa michuano ya wazi ya Ufaransa dhidi ya Pablo Carreno.

Mserbia huyo aliwasili mchezoni akiwa na mkanda shingoni, na mara kadhaa alionekana akipiga bega lake la kushoto huku akijinyoosha shingo kiasi cha kutia wasiwasi na alipoteza seti ya kwanza, lakini akaendelea kushinda seti tatu zilizofuata 4-6 6-2 6-3 6-4.

Ilikuwa ni mechi ya marudiano ya mwezi Septemba huko Amerika kwenye michuano ya wazi ya Marekani, ambapo Djokovic alishindwa kwa kuondolewa mashindanoni baada ya kumpiga na mpira jaji kwenye mstari.

Djokovic ataumana na Stefanos Tsitsipas, katika hatua ya nusu fainali. Endepo atatwaa ubingwa huu atakuwa mchezaji wa kwanza kutwaa kila Grand slam mara mbili.