
Msanii wa BongoFleva Lady Jaydee na Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza
Kupitia mahojiano aliyofanya na EATV & EA Radio Digital, Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano wa BASATA Godfrey Nago amefafanua zaidi kuhusiana na hilo ambapo amesema.
"Kuhusu taarifa hizo naweza kusema nusu zina ukweli na nusu hazina ukweli kwa sababu bado hatujaita mkutano au kuongea na mtu yeyote kwenye hadhara kuhusu suala hilo, kitu ambacho tumefanya ni kumuita yeye kwanza na tayari tumeshampelekea barua kupitia Mwanasheria wetu ambayo anatakiwa aripoti hapa, halafu kuanzia hapo ndiyo tutakuwa na cha kuzungumza naye, huwezi kutoa hukumu kabla hujamzikiliza mtu"