
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kuku wa soko la Shekilango
Wakiongea na EATV wafanyabiashara hao wamesema gari la kuzoa taka limekuwa halipiti mara kwa mara na hivyo kusababisha harufu mbaya inayotokana na manyoya ya kuku kuoza baada ya kuku kuchinjwa na kusema hali hiyo inapaswa kushughulikiwa kwa haraka.
“Harufu hii inatuathiri hata afya zetu kwa kuwa inatokana na mchanganyiko wa takataka ambazo zikioza harufu inakuwa mbaya”amesema Emmanuel Christopher mfanyabiashara wa kuku soko la Shekilango.
Bw. Christopher amesema wameshatoa taarifa kwa uongozi wa manispaa ya Ubungo ili kushughulikia tatizo hilo na wanachosubiria kwa sasa ni utekelezaji wa uzoaji wa taka hizo mara kwa mara ili kuokoa afya za wafanyabiashara na watumiaji wa soko hilo.