
Clatous Chama (Wa kwanza kulia) akiwa mazoezini na wenzake Meddie Kagere( Kati) na Erasto Nyoni( Wa kwanza kushoto) .
Chama amesema, ''ninataka kuelezea ukweli juu ya suala la mimi kutojiunga na timu ya taifa pamoja na mkanganyiko wa mimi kutoripoti kambini, linalohusishwa na mgapngilo wa tarehe ya safari''.
''Sikutaka kusema katika hili lakini nahisi kuna haja ya kufanya hivyo. Kwanza kabisa, nyote mnahitaji kujua na kuelewa kwamba mimi na kocha pamoja na chama cha mpira wa miguu cha Zambia FAZ tuko katika hali nzuri'', ameongeza.
Katika kuendelea kufafanua, Chama ameongeza kuwa, ''sikuwa na wakati wa kumsikiliza kocha leo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari lakini niliongea na msimamizi wa timu juu ya haya yote.
Ukweli ni kwamba sikukosa safari mbili za ndege na niliongea na kocha kabla ya mchezo wetu huko Dodoma na kumuelezea kuwa haiwezekani kwangu kufika kwenye ndege ya kwanza ambayo nilipata sababu ilikuwa saa 3 asubuhi Jumatatu na mchezo wetu ulikuwa saa kumi jioni Jumapili kule Dodoma''.
Kuhusu umbali chama ameendelea kuandika kuwa, ''Umbali kutoka Dodoma hadi Dar ni saa 8 na kwa vyovyote timu haikuwa na mipango ya sisi kusafiri baada ya mechi. Nilipata tiketi Yangu ya pili kwa jana na wakati wa kuondoka ilikuwa 8: 45 asubuhi na wakati nikiwa najiandaa kwa safari yangu, niliambiwa kwamba sipaswi kusafiri''.
Na kwa upande wa watu wa Zambia wanaomlaumu kwa kitendo hicho amewaandikia ujumbe, ''Sikubaliani na Wazambia wengi ambao wanaamini kuwa sina nidhamu vilevile sikukosa ndege yoyote kati ya mbili ambazo nilipata. Asante sana naitakia Timu ya kitaifa mafanikio mema kuelekea mchezo huo''.