
Rais Donald Trump na mkewe Melania.
Trump mwenye umri wa miaka 74, ambao ni wa kundi lililopo kwenye hatari zaidi, ametangaza taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter, huku akisema hali hiyo wanayopitia itapita.
Taarifa hii inakuja baada ya mmoja wa wasaidizi wake wa karibu kubainika kupata maambukizi ya corona.
Hope Hicks mwenye umri wa miaka 31, ni msaidizi wa karibu zaidi wa rais Trump kubainika kupata maambukizi ya corona.
Msaidizi huyo alisafiri naye kwa ndege ya rais Air Force One, kwenye mdahalo wa kwanza wa urais dhidi ya mpinzani wake wa Democratic Joe Biden huko Ohio siku ya Jumanne.
Baadhi ya wanafamilia wa rais Trump waliohudhuria mdahalo huo walionekana wakiwa hawajavaa barakoa.