
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli upande wa kulia, kushoto ni msanii Rose Muhando
Mkutano huo wa hadhara umefanyika Vwawa Mjini katika Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, ambapo Dkt Magufuli alimpatia zawadi ya kofia kama alivyowafanyia wasanii wengine kama Alikiba, Harmonize, Kala Jeremiah, Linex na wengineo.
"Asante Mungu wangu wa mbinguni, asante Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JPM" ameandika Rose Muhando
Kimuonekano na nguvu ambayo aliionesha wakati anaimba kwenye jukwaa imewatoa hofu mashabiki zake ambao walidhani kama bado Rose Muhando anasumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma Rose Muhando alikuwa ana matatizo ya kiafya ambayo yalisababisha watu kuongea mengi kuhusu yeye hadi kufikia hatua ya kwenda kuombewa kwa wachungaji wa Kenya pia kuna muda alionekana akipatiwa maombi kwenye Kanisa la Mlima wa moto chini ya marehemu Bi Gertrude Rwakatare.