
Patrice Evra akiongea na vyombo vya habari
'' Nimelazimika kumjibu Rais wa Shirikisho la soka la Ufaransa Noel Le Graet na kuueleza umma juu ukweli wa jambo hili, nina mifano kadhaa juu ya ubaguzi wa wachezaji wenye asili ya Afrika tuliokuwemo katika timu ya Taifa''
'' Nakumbuka kuna siku Rais wa nchi alitutembelea kambini, kuzungumza na wachezaji wa timu ya Taifa wakati wa kupiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu, pembeni ya Rais upande wa kushoto alikuwa Mamadou Sakho na Bakar Sagna ambao wana asili ya Africa, lakini katika hali ya kushangaza wachezaji hao waliondolewa na kuletwa Hugo Lloris na Laurent Koscielny na Rais kusimama katikati yao'' anasema Evra
NI KWELI KUNA UBAGUZI WA RANGI NDANI YA TIMU YA TAIFA YA UFARANSA?
Ni dhana isiyoweza kuthibitishwa kwa urahisi, kwa kuwa historia inaonesha mchanganyiko wa wachezaji wenye asili ya Afrika katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa umekuwepo tangu enzi hizo, wapo wachezaji waliocheza timu hiyo kwa mafanikio makubwa kama Jean Pierre Adam 1972-76 ambaye alizaliwa Senegal baadaye akaenda Ufaransa, Jean Pierre Tigana 1980-1988 alizaliwa Mali na kwenda Ufaransa
Katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Dunia mwaka 1998 nyumbani Ufaransa kulikuwa na wachezaji zaidi ya 10 katika timu hiyo akiwemo Patrick Viera, Marcel Desail, Thierry Henry Lilian Thuram Zidane nk.Pia katika kikosi kilichotwaa ubingwa 2018 nchini Urusi zaidi ya wachezaji 10 wenye asili ya Africa walikuwemo akiwemo Paul Pogba,Ousman Dembele,Blaise Matuidi,Samwel Umutiti, Ng'olo Kante na wengineo