Tamasha hilo linatarajia kufanyika nchini katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa Bagamoyo ambako pia kutakuwa na warsha kutoka kwa wataalamu mbalimbali toka pembe zote za dunia kwa mujibu wa msemaji wa tamasha hilo, Muslim Nasoro.
Tamasha hilo Isam Ramadhani litafanyika kwa siku Tatu kuanzia Novemba 7-9 Mwaka huu ambapo vikundi zaidi ya 30 na wasanii kutoka kila kona ya dunia wanaopiga muziki wa dansi, Reggae, Hip Hop, Taarab, Ngoma za Asili, Bongofleva na Rap wanatarajia kushiriki.
Tamasha hili litakuwa likitumia ala za muziki na wasanii wote watakaoshiriki watatumia mtindo huo katika uimbaji.