
Kocha wa Namungo, Hitimana Thiery akizungumzia mwenendo wa Timu yake msimu huu.
Thiery kwasasa hawapati matokeo mazuri kwasababu bado wachezaji wengi ni wapya ambao anaendelea kuwatumia ili apate kikosi imara kama cha msimu uliopita.
“Kwakweli bado hatujafanya vizuri kwasababu ni majeruhi wengi kwenye timu yangu ndiyo maanna watu wanaona nabadilisha kikosi kila mechi, wachezaji wangu tegemezi kama Carlos Protas, Edward Charles Manyama wote bado hawajarejea hivyo inanipa shida sana” alisema Kocha wa Numungo Hitimana Thiery.
Mrundi huyo pia amesema kuwa mchezo dhidi ya Mbeya City hautakuwa rahisi kwao kwasababu wapinzani wao hawajashinda mechi yoyote na pia watakuwa na faida ya kucheza katika dimba la nyumbani.
Katika hatua nyingine Hitimana amesema bado hajapata taarifa yoyote kuhusu usajili wa Mlinzi Kelvin Yondan katika Klabu yao lakini pia amesema atafurahia kumuona beki huyo kisiki anajiunga na timu yake kwani ni mchezaji mzuri.