Ummy Mwalimu
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mzizima, Ummy, ameahidi kusimamia uwezeshaji wa kiuchumi kwani utasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake
"Nitasimamia uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake, vijana watu wenye ulemavu pamoja na wajasiriamali wadogowadogo ndugu zangu wana mzizima hiko ndicho kipaumbele changu cha kwanza” amesema Ummy Mwalimu
Aliendelea kufafanua, “Ninaamini tukiwa na kipato cha uhakika hata masuala ya elimu kwa watoto wetu yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili".