Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu
Amesema kuwa hivi Sasa wanawake wamejitokeza kwa wingi akieleza kuwasilisha wazo kwa Waziri wa Fedha na mipango kuondoa ama kushusha riba katika Taasisi za Fedha ili kuwainua wajasiriamali katika Shughuli zao kibiashara.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo August 27 katika mkutano uliowakutanisha wanawake wa Jumuiya ya Africa mashariki kwa kushirikiana Wizara ya Afya na Jukwaa la wafanyabiashara wanawake (TWCC) ambapo amezindua Jukwaa la wanawake milioni 50 wafanyabishara wa kiafrica.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Hicho Jacqueline Maleko ameiomba serikali kuweka Sera ambazo zitasaidia kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi ikwemo kuweka mikopo yenye riba nafuu ili waweze kukuza mitaji yao.
Zaidi ya nchi 38 za Africa Kati ya 54 zimetajwa kuingia katika Umoja huu Ambapo wafanyabiashara wanawake wameaswa kulitumia soko Hilo la mtandao wa wanawake barani Africa uliozinduliwa hii leo.