Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam ambapo wamesisitiza sheria zinazomlinda mlemavu katika ngazi zote za jamii kufuatwa huku wakisisitiza kutekelezwa kwa matakwa hayo utasaidia kuondoa idadi kubwa ya walemavu katika mitaa kama ombaomba.
Wamesema licha ya kuwepo kwa vyombo vinavyosimamia ikiwemo wizara maalumu ya watu wenye ulemavu bado elimu kuhusu namna ya kuwahudumia katika jamii haijasisitizwa ipaswavyo.
“Hili suala la watu wenye ulemavu kushiriki kama ombaomba mtaani limekuwepo na mara zote wanaohojiwa wanaeleza kuwa maslahi yao hayajatatuliwa,ifike wakati ambao wao wenyewe watambue ulemavu sio ugonjwa na wana haki sawa mbele ya sheria” alisema
Akizungumzia kuhusu Sera ya huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu (WWU) Mwanasheriawa masuala ya watu wenye ulemavu Novath Kuwago amesema kuwa ni vyema kundi hilo liweze kupata huduma za afya, elimu jumuishi, kazi na ajira Huduma za utengamo.
Kuwango amesema mbali na Sheria na miongozo iliyopo ipo adhabu inayotolewa ikiwa mtu au taasisi atashindwa kusimamia matakwa ya watu wenye ulemavu kwa makusudi
haswa baada ya mkataba wa kulinda na kuhakikisha wanafurahia kikamilifu na kwa usawa haki zote za msingi za binadamu.
“ Adhabu zipo haswa Iwapo ni mtu binafsi atalipa faini isiyopungua laki 5 na isiyozidi milioni 7 au kifungo cha mwaka au vyote.” alisisitiza