Msemaji Mkuu wa serikali Dkt Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani)
Dkt Abbasi ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitano ambapo miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme nchini kutoka megawati 1,308 mwaka 2015 hadi kufikia megawati 1,602.32 mwaka 2020.
Kwa upande wa mageuzi kwenye Sekta ya Madini amesema “Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa”.
Kwa upande mwingine ni uendelezaji wa ujenzi wa mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia, mradi wenye lengo la kusindika gesi asilia kuwa kimiminika. “jumla ya TZS Bilioni 5.2 imelipwa kwa wananchi 618 kati ya 693 watakaopisha mradi katika eneo la Likong’o, Lindi.”, amesema.
Akielezea mafanikio katika upatikanaji wa umeme wa uhakika, Dkt Abbasi amesema hadi kufikia Julai, 2020 jumla ya vijiji 9,412 vimeunganishwa kutoka vijiji 2,018 mwaka 2015, ikiwa ni sawa na ongezeko la vijiji 7,394 huku akisisitiza uendelezwaji wa miradi mingine kwaajili ya kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.
“Serikali ya awamu ya tano pia imetumia takribani TZS Trilioni 1.109 ya fedha za ndani kutekeleza miradi mikubwa miwili ya umeme wa gesi: Kinyerezi-I Extension megawati 185 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na zaidi ya TZS Bilioni 315.4”.
Dkt Abbasi hakusita kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini ambapo amesema katika mageuzi kwenye Sekta ya Madini. “Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa”.
Amefafanua zaidi na kusema kuwa moja ya mafanikio ya serikali ya wamu ya tano katika Sekta ya Madini hadi Juni, 2020 ni pamoja na kuongezeka kwa masoko ya madini 31 na vituo vya ununuzi wa madini 39 vilianzishwa maeneo mbalimbali nchini.