Sunday , 26th Oct , 2014

Vilabu Saba kutoka mikoa mitatu nchini ya Tanga, Kilimanjaro na wenyeji Dar es salaam vinatarajia kushiriki michuano ya Judo Klabu bingwa Taifa inayotarajiwa kufanyika Novemba 8 katika ukumbi wa Shule ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa Chama cha Judo nchini JATA, Innocent Malya amesema Novemba 7 vilabu hivyo vinatarajia kupima uzito kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo yenye lengo la kuunda timu ya taifa itakayoshiriki michuano ya Judo Kanda ya Tano mwakani Tanzania ikiwa wenyeji wa michuano hiyo.

Malya amesema baada ya mabondia hao kupima uzito, kutakuwa na semina ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo pamoja na wale watakaochezesha michuano ya Kanda ya Tano.

Tags: