Saturday , 8th Aug , 2020

Katika Mkutano wa Baraza kuu la umoja wa vijana UVCCM, uliofanyika leo Agosti 8, 2020, zoezi la upigaji kura wa kupata wabunge wa viti maalumu katika kundi la vijana limemalizika.

Halima Bulembo

Matokeo ya kura za maoni UVCCM Wabunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana Baraza la Wawakilishi nafasi mbili.

Walioongoza ni,

1. Saraham Mohamed kura 66 
2. Hudhaina Mbaraka Kura 50 

Matokeo ya kura za maoni UVCCM Wabunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana Wabunge Zanzibar nafasi nne.

Walioongoza ni, 

1. Munira Khatib kura 88
2. Latifa Juakali kura 84 
3. Amina Baraka Yusuf kura 79
4. Amina Ally Mzee Kura 73

Matokeo ya kura za maoni UVCCM  kupata Wabunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana, Wabunge Tanzania Bara nafasi sita.

Walioongoza ni,

1. Lulu Mwacha kura 77
2. Halima Bulembo kura 74
3. Juliana Masaburi kura 70
4. Lucy John kura 48
5 na 6 wamefungana, Judith Kipenga na Asia Abdukarim kura 33.