Friday , 7th Aug , 2020

Nyota wa zamani wa Vilabu vya Arsenal na Manchester United, Robin Van Persie ametangazwa kuwa ndiye kocha msaidizi katika klabu ya Feyenoord ya Uholanzi.

Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uholanzi na klabu ya Feyenoord

Van Persie ayeliwahi kuichezea timu hiyo akiwa bado kijana mdogo kabla ya kutimkia nchini Uingereza na kurejea tena,sasa atafanya kazi ya usaidizi akiwa chini ya kocha mkuu Dick Advocaat.

Kocha huyo ambaye ameichezea Timu ya Taifa ya Uholanzi michezo 102, aliifungia Feyernood magoli 35 katika michezo 98 aliyoichezea timu hiyo katika vipindi viwili.

Nyota huyo alitundika daruga mwaka uliopita na akawa anajishughulisha na masuala ya uchambuzi wa michezo katika moja ya kituo cha habari nchini Uholanzi.