Monday , 3rd Aug , 2020

Kamati ya tuzo za Ligi kuu Tanzania Bara leo imetangaza wachezaji wanaowania tuzo mbalimbali katika ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/2020 huku kukionekana kuwa na ushindani katika vipengele mbalimbali.

Kiungo wa klabu ya Simba Clatous Chama (Wa mbele katika picha) ,anayepewa kipaumbele cha kubeba tuzo ya kiungo na mchezaji bora.

Katika tuzo hizo zitakazofanyika August 7, Mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Kiungo wa Klabu ya Simba sc Clatous Chama ametajwa kuwania tuzo ya kiungo bora wa msimu pamoja na Mchezaji Bora wa msimu huku ushindani ukiwa katika eneo la mchezaji bora ambapo Chama akiwa anawania sambamba na beki wa Azam FC Nicolas Wadada pamoja na mlinzi wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto.

Kwa ujumla tuzo ziko kama ifuatavyo

Tuzo ya Mchezaji bora
-Clatous Chama-Simba sc
-Nicolas Wadada-Azam Fc
-Bakari Mwamnyeto-Coastal Union

Tuzo ya goli bora
-Sadala Kipangile-(Kmc vs Mtibwa)
-Luis Miquisone-Simba sc vs Alliance Fc)
-Patson Shikala-Mbeya City vs Jkt Tanzania)

Mchezaji bora chipukizi
-Kelvin Kijiri-Kmc Fc
-Dickson Job-Mtibwa Sugar
-Novatus Dismas-Biashara United

Tuzo ya kipa bora
-Daniel Mgore-Biashara United
-Nourdine Balora-Namungo Fc
-Aishi Manula-Simba sc

Tuzo ya kocha bora

-Sven Vandebrook-Simba sc
-Hitimana Thiery-Namungo
-Aristica Cioaba-Azam fc

Tuzo ya timu yenye nidhamu
-Mwadui fc
-Kagera Sugar
-Costal Union