Wednesday , 29th Jul , 2020

Msemaji wa klabu ya Ruvu shooting Masau Bwire amesema kitendo au kauli alizoongea aliyekua kocha wa Yanga ni za kulaani na sio kuzitumia kama utani.

Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire akiwa Studio za East Africa Radio katika Kipindi cha Kipenga kujadili masuala mbali mbali ya Michezo.

Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha KIPENGA kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2 usiku, Masau amesema, hajui kwa sasa kocha huyo (Eymael) yuko wapi "na mpaka sasa vyombo vya usalama nchini vilitakiwa viwe vimemfukuza Tanzania.

Bwire amesema anasikitishwa sana na baadhi ya mashabiki wanaofikia hatua ya kusema kuwa kama wao ni Simba kunatatizo gani kwa Yanga kuwa Nyani kwani wote ni wanyama.

Ameeleza kauli hizo ni za kibaguzi na hazifai kutumiwa kama utani kwani waliutukanwa sio Yanga pekee bali ni nchi nzima ya Tanzania, na pia mataifa mengine nje hayajui kuwa ni Yanga ndio walioitwa nyani bali wanajua ni watanzania ndio waliobaguliwa kwa kuitwa jina hilo.