Shirikisho la watu wenye ulemavu nchini SHIVYAWATA limeibuka na kusema kuwa katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupigiwa kura na wananchi haipo kwa maslahi ya taifa bali inalinda watu wachache wenye nguvu na kuacha mambo mengi ambayo yalipendekezwa na shirikisho hilo.
Kauli hiyo imetolewa mjini Musoma na mjumbe wa bodi ya shirikisho hilo nchini Bw Batista Mgumu, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kujadili wa haki na usawa kwa watu wenye ulemavu mkoa wa Mara na kushirikisha wakuu wa idara mbalimbali za serikali na sekta binafsi mkoani mara.
Amesema SHIVYAWATA iliwasilisha kwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba maoni mengi yenye maslahi pia kwa watu wenye ulemavu ukiwemo uwakilishi katika vyombo vya maamuzi, lakini cha kushangaza katiba hiyo pendekezwa imepuuza baadhi ya maoni hayo.
Thursday , 23rd Oct , 2014
Shirikisho la watu wenye ulemavu nchini SHIVYAWATA limeipinga Katiba Inayopendekezwa kwa madai kuwa imeacha mambo mengi muhimu kwa walemavu.