Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Julai 22, 2020, wakati wa uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jijini Dodoma.
"Ninaamini vyama vyote vitafanya kampeni kistaarabu, basi tukawe wavumilivu na niviombe vyombo vya dola visitumie nguvu pasipostahili, lakini hata nyinyi wanasiasa msiwachokoze wale walinda amani, msiwafanye watumie nguvu" amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 28, itakuwa ni siku ya mapumziko hivyo itatangazwa rasmi.


