Arsenal na Man City
Mabingwa watetezi Manchester city wataonyeshana umwaba dhidi ya mabingwa wa kihistoria Arsenal ambao ni mabingwa mara 13 wa michuano hii ya FA na hii ni kwa mara ya 30 wanafika katika hatua ya nusu fainali wakiwa wamecheza fainali mara 20. Man city wametwaa taji hili mara 6 tu.
Kikosi cha kocha Mikel Arteta hakijawa na matokeo mazuri mbele ya Manchester city kwa miaka ya karibuni, takwimu zinaonyesha Arsenal wamepoteza michezo 7 ya mwisho waliokutana na Manchester city katika michuano yote wakiruhusu mabao 20 katika michezo hiyo huku wao wakifunga mabao 2 tu.
Mara ya mwisho Arsenal kuifunnga Manchester city ilikuwa kwenye hatua kama hii ya nusu fainal ya FA mwaka 2017 ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Arsenal wataingia kwenye mchezo huu wakiwa hawana mchezaji mpya mwenye majeruhi zaidi ya wale wa muda mrefu ambao ni Pablo Mari kifungo cha mguu, Bernd Leno, Gabriel Martinell na Calum Chambels wato wanamajerui ya goti, lakini pia habari njema kiungo mchezeshaji Mesut Ozil amerejea mazoezini wiki hii baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kwa maumivu ya mgongo, ni maamuzi ya kocha Mikel Arteta kama ataona Ozil yupo fiti kucheza.
Kocha wa Man city Pep Guardiola atamkosa Claudio Bravo ambaye amekuwa goli kipa namba moja kwenye michuano hii ataukosa mchezo huu kutokana na maumivu ya misuli, lakini pia mshambuliaji Sergio Kun Aguero ni mchezaji mwingine atakae kosekana kwenye kikosi cha Manchester city.
Mshindi wa mchezo huu atakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili itakayochezwa kesho july 19 kati ya Manchester United dhidi ya Chelsea.

