Wednesday , 22nd Oct , 2014

Mabondia nchini wametakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiimarisha kwa ajili ya mashindano mbalimbali yaliyopo mbele yao.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu mkuu wa Shirikisho la Ngumi nchini PST, Antony Ruta amesema mabondia Kalama Nyilawila,Mada Maugo na Ramadhan Shauri ambao walishindwa kufanya vizuri katika pambano lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Urusi la kuwania Ubingwa wa WBC walishindwa kufanya vizuri kutokana na kushindwa kufanya maandalizi mapema.

Ruta amesema mabondia mbalimbali hapa nchini wamekuwa na mazoea ya kufanya mazoezi wanaposikia wanamashindano suala linalopelekea kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.