Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, na Mwanachama wa ACT Wazalendo, Bernard Membe.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 17, 2020, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, hii ni baada ya hapo jana wanachama wa chama cha ACT Wazalendo, kumuomba awanie nafasi hiyo kwa lengo la kuleta ustawi na maendeleo kwa Taifa.
"Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama CHADEMA ili tusimamishe 'Kisiki cha Mpingo' kimoja!" ameandika Membe.
Jana wakati akizungumza na wanachama wa ACT Wazalendo, alieleza ni kwa namna gani alifedheheshwa, baada ya kufukuzwa uanachama na CCM, "Mimi nimefukuzwa tena kwa aibu na kutukanwa na vijana ambao ningeweza kuwazaa, na sikutenda kosa lolote hata mbele ya Mungu, kosa nililofanya ni la kugombea Urais 2015, milango imefungwa na kufunguliwa na ACT na nikakaribishwa chumbani".